Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya shindano la (Mazazi ya Shaabaniyya matukufu) la kitamaduni

Maoni katika picha
Kutokana na mazazi matukufu yaliyotokea katika mwezi wa Shabani, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unaendesha shindano la (Mazazi ya Shaabaniyya matukufu), unaweza kushiriki kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/1H8Zj1or4UkGmTQJ6.

Majina ya wenye majibu sahihi yatatangazwa jioni ya siku ya Jumamosi tarehe (5/3/2022m), washindi kumi na tano miongoni mwao watapatikana kwa kupiga kura moja kwa moja siku ya hafla, baada ya mshiriki mwenye jibu sahihi kufika katika vituo viwili vitukufu, ambavyo ni:

Kwanza: Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake lililopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu mlango wa dhahabu/ mkabala na mlango wa Imamu Aljawaad (a.s).

Pili: Kituo cha mahusiano katika kitengo cha Habari nacho ni maalum kwa wanaume, kipo upande wa mlango wa Imamu Ali (a.s).

Hafla hiyo itafanywa siku ya Jumapili tarehe (6/3/2022m) kuanzia saa tisa mchana hadi saa kumi na moja jioni, sharti la kupokea zawadi, mshiriki anatakiwa awepo kwenye hafla hiyo, awe na kitambulisho chenye majina yake na picha yake, asipokuwepo au akawa hana kitambulisho atachaguliwa mshindi mwingine kwa njia hiyohiyo ya kura.

Tambua kuwa zawadi ya pesa ni (250,000) laki mbili na elfu hamsini dinari za Iraq na mfuko wa zawadi za kutabaruku kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Tunawatakia mafanikio mema washiriki wote kwenye shindano hilo na kwenye shughuli zao zingine za kiimani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: