Shule za Alkafeel za wasichana kitengo cha Dini zimeandaa ratiba mbalimbali za watoto

Maoni katika picha
Idara ya shule za Alkafeel za wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa ratiba ya watoto katika shule zake za ndani na nje ya mji wa Karbala.

Kiongozi wa idara bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Idara ya shule inaharakati nyingi, haishii kufundisha Dini peke yake, bali inaratiba zingine zinazolenga kundi la wasichana na watoto wa kike”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba iliyo andaliwa kwa wasichana hao ambayo ni muendelezo wa hatua zingine, inaendana na umri wao na kiwango cha elimu waliyo nayo, imekua na matokeo chanya, sambamba na kuzingatia mbinu za kufikisha elimu, chini ya wasimamizi mahiri wenye uzowefu mkubwa katika sekta hiyo”.

Akabainisha kuwa: “Vipengele muhimu vya ratiba ni: Akhlaq, malezi, Qur’ani, Mahdawiyya, historia ya Ahlulbait (a.s), sambamba na kubaini vipaji na kazi za mikono na mengineyo yanayo saidia kuongeza elimu”.

Program hiyo imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wazazi, wamesema hili ni jambo zuri, linasaidia kujenga binti zao. Wakatoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na wasimamizi wa mradi huo.

Kumbuka kuwa shule zilizo fanya ratiba hiyo ni (Zainabu bint Ali, watakasifu wadogo, Rihanatu-Mustwafa, Nuru-Zaharaa, Alhauraa, Ummu-Abiha, Bidh’atu-Twahirah (a.s)). Kutokana na muitikio mkubwa uliopatikana, idara itaandaa program nyingine itakayo husisha idadi kubwa ya shule.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: