Kabla ya usiku wa furaha: Usafi mkubwa unafanywa katika eneo linalo zunguka ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu toka mapema asubuhi ya leo siku ya Ijumaa, wanafanya usafi mkubwa katika eneo linalozunguka ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na baadhi ya barabara zinazo elekea haram.

Usafi ni moja ya shudhuli zinazofanywa na watumishi hao kila siku, leo wanafanya usafi mkubwa kutokana na mji wa Karbala kupatwa na kimbunga cha udongo jana, sambamba na maandalizi ya kupokea mwezi mtukufu wa Shabani na kumbukumbu ya mazazi matukufu.

Kazi hiyo inafanywa na watumishi wa idara ya usafi, wameanza kusafisha eneo linalozunguka Ataba kwa nje na barabara zinazo elekea haram, pamoja na sehemu za vibaraza, bustani na vituo vya maji ya kunywa, kazi hiyo inafanywa kwa kutumia mitambo na juhudi za binaadamu, wamefanikiwa kumaliza kazi ya kusafisha maeneo yote na hali kurejea kama ilivyo kuwa awali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: