Mazingira ya furaha yametanda katika Atabatu Abbasiyya kufuatia kuingia kwa mwezi mtukufu wa Shabani, mwezi wenye matukio muhimu kwa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), kumbukumbu ya kuzaliwa miezi ya Sha’abaniyya (a.s).
Ukumbi mtukufu wa haram umepambwa vitambaa vilivyo andaliwa na wahudumu wa kitengo cha zawadi na nadhiri, na kuandikwa maneno mazuri yanayo ashiria furaha kubwa ya waumini katika mwezi huu mtukufu.
Kazi hiyo ilitanguliwa na kupamba dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa shada za mauwa, kisha kazi ikaendelea ya kupamba kila sehemu ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba kamili ya kupokea mwezi wa Shabani na mambo matukufu yaliyotokea katika mwezi huo, kuanzia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s) tarehe tatu Shabani, na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) tarehe nne na mwanae Imamu Sajjaad Zainul-Aabidina (a.s) tarehe tano, mwisho kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Imamu wa zama (a.f), tarehe kumi na tano, bila kusahau kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Ali Akbaru mtoto wa Imamu Hussein (a.s) tarehe kumi na moja mwezi huu.