Kuanza kwa kongamano la kiongozi wa wasomaji la wasichana kwa mara ya kwanza

Maoni katika picha
Jioni ya Ijumaa shughuli za kongamano la kiongozi wa wasomaji wasichana zimeanza kwa mara ya kwanza, linalo simamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani katika Majmaa ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kongamano hilo limefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, mbele ya katibu mkuu na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo, pamoja na kundi la wanafunzi na walimu wa hauza na sekula.

Tumeongea na rais wa Majmaa ya Qur’ani Dokta Ahmadi Sheikh kuhusu kongamano hilo, amesema: “Kongamano hili linaimarisha uwelewa wa wazazi wa wanafunzi wanaoshiriki kwenye mradi, na linatoa picha halisi ya fikra ya kusambaza utamaduni wa kujali Qur’ani”.

Akaongeza kuwa: “Mradi huu ni moja ya miradi inayofanywa kila mwaka, tunakusudia kuwapa vijana muelekeo sahihi na salama kupitia Qur’ani tukufu na muongozo wa kizazi kitakatifu”.

Naye mkuu wa kituo cha miradi ya Qur’ani Hasanaini Halo amesema: “Kongamano hili limefanywa baada ya tatizo la Korona, kwa lengo la kuendelea na harakati za Qur’ani zilizokua zimeanza kutekelezwa toka mwaka 2013m”. akaongeza kuwa: “Kongamano hili ni kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wanafunzi na wazazi wao bila kusahau walimu wa vituo vya ufundishaji wa Qur’ani vya Iraq, vyenye jukumu la kuwafundisha na kuwaendeleza kupitia mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa”.

Akafafanua kuwa: “Katika kongamano hili tunakusudia kufungua majadiliano kati ya wazazi na viongozi wa taasisi, kwa ajili ya kuboresha ufundishaji wa njia ya mtandao katika mradi huu na kozi za kimtandao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: