Chuo kikuu Alkafeel kimefungua milango yake na kuruhusu watu kutembelea bustani zake

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetandaza kufunguliwa milango yake kwa ajili ya kupokea familia za wairaq wanaokuja kutembelea na kupumzika katika bustani zake siku hizi za kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi matukufu ya Shaabaniyya.

Dokta Nawaal Almayali makamo rais wa chuo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya Mheshimiwa rais wa Chuo Dokta Nuris Dahani, kufuatia maadhimisho ya mazazi matukufu ya Shaabaniyya, bustani za chuo kikuu cha Alkafeel zitafunguliwa kwa ajili ya wananchi watukufu, ili waje kukaa na kupumzika kwenye eneo hilo, kwani chuo kinaeneo kubwa la bustani linaloweza kuingiza watu wengi”.

Akaongeza kuwa: “Tutaanza kupokea watu siku ya kwanza ya mwezi wa Shabani hadi siku ya kumi, kuanzia saa kumi asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni, bustani zote zimewekwa tayali na mauwa yake yamepangiliwa vizuri, ni sehemu bora ya kukaa na kupumzika”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kinaeneo kubwa la bustani, lenye mazingira mazuri ya kujisomea na kupumzika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: