Idara ya faharasi katika kituo cha turathi za Basra imefanya kazi kubwa ya kuhifadhi turathi za mji wa Nafisi

Maoni katika picha
Idara ya faharasi katika kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, ni moja ya idara maalum ya kuhuisha turathi za kitamaduni na nakala-kale za mji wa Basra.

Idara imefanya kazi kubwa yenye mafanikio mazuri, imeweza kufanyia utafiti turathi nyingi na kuzitunza.

Idara hiyo inajukumu la kukusanya nakala-kale za Basra kutoka sehemu tofauti, kama vile (kwenye maktaba mbalimbali), au kutafuta kwenye mitandao, kisha idara huchambua nakala-kale hizo na kuziweka kwenye faharasi baada ya kuzihakiki, sambamba na kukusanya taarifa za wanachuoni wa Basra na kutafuta turathi zao za nakala-kale.

Kazi inaendelea hivi sasa katika idara hiyo kwa ushirikiano mkubwa kama nyuki, nakala-kale zote walizoibua zinatengenezewa utambulisho na kusajiliwa, ili kurahisisha upatikanaji wake kwa watafiti na mazuwaru.

Tambua kuwa kituo cha turathi za Basra kipo mstari wa mbele katika kuhuisha na kuthibitisha turathi za Basra, na kudhihirisha hazina zake ambazo ni urithi wa kihistoria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: