Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Shaabaniyya

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu joini ya Jumapili kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s), imefanya hafla ya kuhuisha kuzaliwa kwa miezi ya Shaabaniyya, itakayo endelea kwa muda wa siku tatu.

Hafla hiyo iliyofanywa katika ukumbi wa mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na idadi kubwa ya viongozi na marais wa vitengo na watumishi wao, bila kusahau wageni waalikwa kutoka sehemu tofauti na kundi kubwa la mazuwaru.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ammaar Alhilliy, ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliowasilishwa kwa niaba na rais wa kitengo cha Dini Shekhe Swalahu Karbalai, alianza kwa kupongeza wahudhuriaji na umma wa kiislamu kwa kuadhimisha tukio hili.

Akafafanua kuwa: “Imamu Hussein (a.s) ni sawa na maneno ya Mwenyezi Mungu yasiyoisha hata kama maji ya bahari yatakua wino, yeye ni Qur’ani isemayo, akasisitiza umuhimu wa kumjua Imamu Hussein (a.s), kwani kumjua kunaweza kusaidia kupata uombezi wake siku ya kiyama”.

Akabainisha: (Umuhimu mkubwa wa kufanya ziara kwa Maimamu watakatifu katika mwezi wa Shabani, sambamba na kutambua mwenendo wa Ahlulbait (a.s) katika nyanja tofauti).

Baada ya hapo zikasomwa kaswida na washairi wa Ahlulbait (a.s), ambao ni (Muhammad Fatwimiy na Abu Fatuma Abudi), kulikua na kipengele cha ngonjera zilizo fanywa na Hussein Akili na Muhammad Amiri.

Kisha igapigwa kura ya wazi kwa wenye majibu sahihi walioshiriki kwenye shindano la wazawa wa Shaabaniyya watukufu, lililosimamiwa na kitengo cha Habari pamoja na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kupatikana washindi kumi na tano.

Tunatarajia hafla itaendele kesho siku ya Jumatatu ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na itakua na vipengele tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: