Kukamilika kwa matokeo ya shindano la (Pambo la Dini) la tafiti za kielimu kwa wanawake

Maoni katika picha
Kitengo cha tafiti za Qur’ani katika chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) cha wasichana, chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimekamilisha shindano la kielimu la (Pambo la Dini) la tafiti za kielimu kwa wasichana lililofanywa siku za nyuma.

Rais wa kitengo tajwa Ustadh Ali Albayati ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Hili ni moja ya mashindano mengi yanayo simamiwa na kitengo, linalenga kukuza kipaji cha kufanya tafiti kwa wasichana, mada zilizo shindaniwa zilikua zinahusu njia za kutekeleza usia wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani kwa vijana waumini, faida ya kujifundisha Qur’ani tukufu na kuihifadhi na kuongezeka elimu katika jamii”.

Akaongeza: “Tunatarajia kuendelea kufanya mashindano ya aina hii, kwa lengo la kushajihisha watafiti wa kike na kuongeza uwezo wao, kwenye shindano hili wameshiriki watafiti wengi kutoka ndani na nje ya Iraq, kamati ya majaji imechagua tafiti bora (5) za watafiti wafuatao:

Mshindi wa kwanza: Rajaa Karim Daghibji, kutoka Iraq.

Mshindi wa pili: Sara Rahim Hamza, kutoka Iraq.

Mshindi wa tatu: Zaharaa Jabbaar Ali, kutoka Iraq.

Mshindi wa nne: Salma Muhammad Shaquul, kutoka Sirya.

Mshindi wa tano: Turkiya Haliil Swiyaah, kutoka Iraq.

Kumbuka kuwa kitengo kimeandaa mashindano ya aina tofauti na ratiba ya Qur’ani itakayo simamiwa na chuo kikuu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: