Watumishi wa Saaqi wanawapongeza watumishi wa mjukuu wa Mtume katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake

Maoni katika picha
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamewapongeza watumishi wa Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Wamefanya hivyo kupitia matembezi yaliyo anza baada ya Adhuhuri ya leo siku ya Jumatatu tarehe (3 Shabani) ndani ya ukumbi wa haram ya Mwezi wa bani Hashim (a.s), yaliyo ongozwa na jopo la viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wakiwa wamebeba mauwa na kuimba kaswida nzuri zinazo onyesha kilele cha furaha yao inayo endana na furaha ya waumini wote katika kuadhimisha siku hii tukufu, na kundi la mazuwaru limeshiriki katika matembezi hayo.

Baada ya kuwasili katika malalo ya baba wa watu huru (a.s) wakapokewa na ndugu zao watumishi wa malalo ya Imamu Hussein (a.s), wakafanya ibada ya ziara kwa pamoja na kuweka mashada ya mauwa juu ya dirisha la malalo ya mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) wakiwa wamejaa shangwe na furaha.

Kisha wakaenda kumpa pongezi Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya tukufu Shekh Abdulmahadi Karbalai, naye alitoa huduba ya ukaribisho na akapongeza maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s), akasisitiza umuhimu wa wahudumu wa Ataba tukufu kufanya kila wawezalo katika kutumikia Maimamu watakasifu na mazuwaru wao, akawatakia mafanikio mema watumishi wote wa Ataba tukufu.

Wakahitimisha ziara yao kwa kukutana na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu Ustadh Hassan Rashidi Al-Abaaiji, na wakampongeza kwa kumbukumbu ya kuzaliwa miezi ya Shaabaniyya, hususan kuzaliwa kwa Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: