Kwa siku ya pili mfululizo: Hafla ya kusherehekea kuzaliwa kwa miezi ya Shaabaniya inaendelea

Maoni katika picha
Jioni ya Jumatatu mwezi (3 Shabani) hafla imeendelea kwa siku ya pili, chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi ya miezi ya Shaabaniyya.

Hafla ya siku ya pili iliyofanywa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi, imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na msomi wa Atabatu Abbasiyya Muhammad Ridhwa Salmaan, ukafuata ujumbe elekezi uliotolewa na Shekhe Harith Dahi kutoka kitengo cha Habari na utamaduni, amepongeza umma wa kiislamu kwa kumbukumbu ya mazazi ya Shaabaniyya, akabainisha nafasi kubwa waliyonayo mbele ya Mwenyezi Mungu watukufu waliozaliwa katika mwezi huu, hususan Imamu Hussein (a.s), akahimiza umuhimu wa kufanyia kazi maneno ya Maimamu watakasifu, maneno yao ni muongozo Madhubuti na njia ya kuokoka duniani na akhera, akaongea pia kuhusu nafasi ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kazi kubwa aliyofanya katika kumnusuru Imamu wa zama zake ndugu yake bwana wa vijana (a.s).

Baada ya hapo muimbaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Ammaar Hilliy Saaidiy akaburudisha masikio ya wahudhuriaji, akasoma maneno matukufu kutoka katika kitabu kitakatifu, kupitia kikao cha usomaji wa Qur’ani kilicho andaliwa kwa siku ya pili ya hafla hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: