Kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s): Miaka saba iliyojaa mafunzo ya elimu na utamaduni kwa wasichana

Maoni katika picha
Miaka saba iliyopita katika siku kama ya leo mwezi (4 Shabani 1436h) katika kumbukumbu ya kuzaliwa mwezi wa bani Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s), kilifunguliwa kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) kwa ajili ya kuendesha harakati za wanawake.

Mradi huu ulianzishwa kutokana na Imani ya Atabatu Abbasiyya ya umuhimu wa nafasi ya mwanamke katika familia na jamii, na umuhimu wa kumuongoza kwa kufuata mafundisho na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), katika njanja zote za kimalezi na kijamii, ili kutoa mchango wake katika kujenga jamii.

Kituo kilichopo katika mkoa mtukufu wa Karbala, ni mradi maalum unaosimamiwa na Ataba tukufu, unaolenga kukuza nafasi ya mwanamke kulingana na umuhimu wake hapa Iraq, na ushiriki wa mwanamke katika sekta tofauti za maisha, sambamba na mafundisho ya Dini ya kiislamu na mtazamo wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s).

Kituo hiki pamoja na kujikita katika shughuli za wanawake, kinahusisha pia (kituo cha utamaduni wa familia – umoja wa wanawake – shule za Alkafee za Dini za wasichana- idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wakike), yote hayo yanalenga kumuendeleza mwanamke kielimu na kitamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: