Ugeni kutoka Atabatu Husseiniyya tukufu unaohusisha wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo pamoja na kundi la wahudumu wake, wamekuja kutoa pongezi kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), ambayo inasadifu leo mwezi nne Shabani, ndani ya malalo yake tukufu.
Ugeni huo umetokea katika malalo ya Abu Adillahi Hussein (a.s), baada ya kutoa pongezi kwake wakiwa wamebeba shada za mauwa, kisha wakaelekea kwenye malalo ya ndugu yake mbeba bendera na burudisho wa macho yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakapitia katikati ya uwanja wa haram mbili tukufu.
Wakapokewa na watumishi wa malalo tukufu wakiongozwa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi, na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria na baadhi ya marais wa vitengo, ugeni huo ukapokewa kwa maneno mazuri ya ukaribisho, sambamba na kutoa pongezi kufuatia maadhimisho haya matukufu.
Kisha wakaenda kwa pamoja kuweka mashada ya mauwa kwenye dirisha la kaburi tukufu baada ya kumaliza ibada ya ziara, wakaongea maneno mazuri ya pongezi na kuomba dua.
Baada ya hapo ugeni ulikutana na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussawi Ahmadi, ukatoa pongezi kutoka kwa wahudumu wa Atabatu Husseiniyya tukufu, akiwemo kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai (d.i) kwa watumishi wote wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wakiogozwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi katika maadhimisho haya matukufu.