Familia na Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika mji mtukufu wa Madina ilipokea kwa shangwe na furaha taarifa ya kuzaliwa kwa Imamu wa nne Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s).
Mwezi tano Shabani mwaka wa (38) hijiriyya, aliye eneza elimu na hekima duniani, mwenendo wake umejaa mafundisho mengi ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.
Mama yake Imamu Sajjaad (a.s) anaitwa Shaha Zanaan mtoto wa Yazdajuridi mtoto wa Shahriyari mtoto wa Kisra, inasemekana jina lake ni Shahribanu, na mke wake ni bibi Fatuma mtoto wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), laqabu zake ni: Zainul-Aabidina, Sayyidul-Aabidina, Sajjaad, Dhuthafanaat, Imamul Mu-uminina, Zaahidu, Al-Amiin, Almujtahidu, Azakiy… na mashuhuri zaidi ni Zainul-Aabidina. Na anakunia zaidi ya moja, miongoni mwa kunia hizo ni: Abu Muhammad, Abul-Hassan, Abul-Hussein, Abu Qassim.
Riwaya zinaonyesha kuwa siku aliyozaliwa (a.s) babu yake kiongozi wa waumini au baba yake Imamu Hussein (a.s), alifanya haraka kumuadhinia katika sikio la kulia na kusoma iqama kwenye sikio ya kushoto, sauti hiyo ilikua mbegu iliyostawi kwa hisia za uchamungu na wema, ilikua sawa na mashine iliyomsukuma katika kufanya wema.
Hakika jambo la kwanza alilokutana nalo Imamu Zainul-Aabidina hapa duniani ilikuwa sauti isemayo (Allahu Akbaru), sauti hiyo ilimjenga na kuishi katika dhati yake, siku ya saba toka kuzaliwa kwake, baba yake alimfanyia hakika na akanyoa nywele zake na kutoa sadaka ya fedha au dhahabu kwa masikini kulingana na uzito wa nywele hizo.
Aliishi (a.s) miaka hamsini na saba, miaka miwili aliishi chini ya uangalizi wa babu yake Imamu Ali (a.s), kisha akaendelea kuishi chini ya Ammi yake Hassan na baba yake Hussein (a.s) wajukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akasoma kutoka kwao elimu tukufu ya utume na maadili matakatifu ya Ahlulbait (a.s).
Shekhe Mufidu katika kitabu cha Irshadi anasema: Ali bun Hussein (a.s) alikuwa mtu bora mbele ya Mwenyezi Mungu baada ya baba yake, wanachuoni wote wamepokea kutoka kwake elimu kubwa isiyokua na mfano, wamehifadhi mawaidha, dua, utukufu wa Qur’ani, halali na haram na vitu vingine vingi mashuhuri kwa wanachuoni.
Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alitokeza katika dunia kama Imamu wa Dini na kinara wa elimu na mfano bora kwa ibada na uchamungu, waislamu wote wanakubali ukubwa wa elimu yake na msimamo wake.
Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alikuwepo katika siku ya Ashura, Mwenyezi Mungu aliamua kuihifathi familia ya Mtume (s.a.w.w) na kuhakikisha dunia haikosi Imamu.
Amani iwe juu ya Zainul-Aabidina na burudisho la jicho la watazamao siku aliyozaliwa na siku aliyouawa na siku atakayo fufuliwa kuwa hai.