Kuanza kwa mchuano wa shindano la Aqmaaru-Shaabaniyya la Qur’ani kwa ushiriki wa vikundi 15

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, limeanza mchuano wa shindano la Shaabaniyya awamu ya kwanza, linalo husiana na usomaji, kuhifadhi, tafsiri, fiqhi na kaswida, kwa ushiriki wa vikundi 15.

Shindano limefanywa katika mji uliopo umbali wa kilometa 20 kutoka makao makuu ya mkoa wa Karbala, lilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Yusufu Fatalawi, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehem mashahidi watukufu wa Iraq.

Ukafuata ujumbe wa tawi la Maahadi ulio wasilishwa na kiongozi wake Sayyid Haamid Mar’abi, alianza kwa kukaribisha wahudhuriaji na washiriki ambao ni vikosi (15), kila kikosi kikiwa na washiriki watano, aidha ameshukuru msaada wa Atabatu Abbasiyya katika harakati za Qur’ani hapa wilayani.

Halafu ukafuata ujumbe wa mkuu wa Maahadi ya Qur’ani Shekh Jawadi Nasrawi, amewakaribisha wahudhuriaji na kupongeza maadhimisho ya mazazi ya miezi ya Muhammadiyya, pia ameshukuru idara na watumishi wa tawi la Maahadi kwa kufanya harakati mbalimbali za Qur’ani, zenye kunufaisha jamii na kujenga utamaduni wa kutambua vizito viwili vitukufu.

Baada ya hapo kukawa na usomaji wa kaswida, zilizo somwa na Abbasi Faadi, ameimba kuhusu kumpenda Mtume na watu wa nyumbani kwake watakatifu (a.s).

Ukafuata upigaji wa kura kwa ajili ya kupata washindi, kikosi cha Habibu bun Mudhahiri na Anwaru-Mustwafa wakaibuka washindi, mshindi wa kwanza alipata kura (72,5).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: