Kwa mara ya kwanza katika masomo ya hauza za wasichana: Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha jukwaa la (Ummul-Banina) la kufundisha Dini kwa elimu masafa

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) cha wasichana katika mji wa Najafu chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimezindua jukwaa la (Ummul-Banina la kusomeshea), nalo ni jukwaa la kielimu la kimataifa lililoandaliwa na kituoa cha Alkafeel cha elimu na teknolojia chini ya chuo kikuu cha Alkafeel.

Mkuu wa chuo Shekhe Hussein Turabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Jukwaa hili ni kwa ajili ya kuendana na maendeleo yaliyopo katika sekta ya ufundishaji kwa njia ya mtandao, kwa kutumia njia za kisasa na kunufaika na teknolojia, jambo hili litawezesha idadi kubwa ya wasichana kushiriki kwenye madarasa ya Qur’ani na Tablighi kutoka sehemu tofauti duniani”.

Akaongeza kuwa: “Masomo yote na mihadhara ya video ya kitengo cha masomo ya Qur’ani na kuandaa mubalighaat yapo kwenye jukwaa, na vitu vingi vyenye uhusiano na mfumo wa chuo (kiidara na kitaaluma), jukwaa hili limefanikiwa kuondoa masafa na kuwaweka wanafunzi karibu”.

Akafafanua kuwa: “Jukwaa litakua tayali kuanzia mwezi wa Shawwal ujao, wakati wa kuanza mwaka mpya wa masomo katika chuo, tunatarajia jukwaa hili litasaidia kurahisisha usomaji wa Dini kwa wale waliokua na ugumu wa kuhudhuria darasani ndani na nje ya Iraq, hususan waliopo Ulaya, Afrika na sehemu zingine”.

Akasema kuwa: “Masomo yatakua bure” akasisitiza kuwa “Kuanzishwa kwa jukwaa hili kunatokana na mpango wa chuo wa muda mrefu, app ya jukwaa hilo itapatikana kwenye program zote (android) na (iOS) na (windows)”.

Unaweza kupakua jukwaa kwa kubonyeza:

Bonyeza hapa: android

Bonyeza hapa: iOS

Bonyeza hapa: windows
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: