Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake yahitimisha shindano la bibi Fedha la Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imehitimisha shindano la bibi Fedha la Qur’ani la kitaifa.

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi amesema: “Baada ya kupatikana wanafunzi (56) wa kushiriki kwenye shindano la bibi Fedha, kilifanywa kikao cha mwisho cha kushindanisha wanafunzi hao walio hifadhi, katika ofisi za kituo kwenye mji wa Najafu na kwenye matawi yetu ya mikoani” akaongeza kuwa: “Tukapata washindi (18) waliohifadhi Qur’ani tukufu, kulingana na makundi yaliyo pangwa kwenye shindano”.

Tambua kuwa Maahadi inaendelea kufanya semina za Qur’ani, sambamba na harakati zingine zinazo lenga kuimarisha utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii ya wasichana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: