Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi, wameanza hatua ya pili ya kupanua uwanja kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru.
Eneo linalo ongezwa kwenye uwanja wa haram lipo Jirani na uzio wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kati ya mlango wa Furaat na mlango wa Imamu Ali (a.s) upande wa mashariki ya Ataba.
Kwa mujibu wa wasimamizi wa kazi hiyo, ujenzi unaofanywa ni kupanua eneo la uwanja, sambamba na kuondoa mabaki ya ubomoaji na kusawazisha uwanja.
Awamu ya tatu itahususha ujenzi wa miundombinu ya (umeme – njia za mawasiliano – kamera – maji safi ya kunywa), pamoja na vitendea kazi katika utoaji wa huduma kulingana na kila aina ya huduma kama zilivyo pangwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kazi hiyo itahitimishwa kwa kuweka marumaru kwenye uwanja huo wenye mamia ya mita za mraba, na kuanza kutumiwa na mazuwaru baada ya kukamilika mambo yote yanayo hitajika kwa zaairu, na kusaidia kupunguza msongamano katika uwanja wa haram tukufu wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.