Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na Maahadi ya afya katika mkoa wa Waasit, imefanya kongamano la wazawa wa Shaabaniyya na kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu, asubuhi ya leo Jumatatu katika uwanja wa Maahadi, na kuhudhuriwa na wakufunzi wengi pamoja na wanafunzi, watumishi na wageni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kongamano hilo limefanywa kwa kushirikiana na idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule katika kitengo cha mahusiano chini ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu na usomaji wa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba tukufu (Lahnul-Ibaa).
Ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na Shekhe Hussein Manahi kutoka kitengo cha Habari na utamaduni, ameeleza baadhi ya usia wa Marjaa Dini mkuu kwa vijana, ukizingatia kuwa wao ndio wajenzi wa taifa hili, vivyo wanatakiwa kupambika kwa elimu na maadili mema, sambamba na kuwa na moyo wa kushindana katika masomo, aidha emeeleza kuhusu mambo yanayo husu ziara ya mwezi kumi na tano Shabani.
Halafu ukafuata ujumbe wa mkuu wa Maahadi Ustadh Ahmadi Hassan Ajiil, ameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na wasimamizi wake kwa kuja kushirikiana nao katika furaha hii tukufu pamoja na utowaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri.
Halafu Atabatu Abbasiyya ikagawa zawadi kwa wanafunzi waliopata nafasi za kwanza katika vitengo vya Maahadi kutoka hatua zote.
Mwisho wakatoa midani na vyeti vya ushiriki baina ya Ataba tukufu na viongozi wa Maahadi, wito ukatolewa wa kuendelea kufanya harakati kama hizi.