Kitengo cha maadhimisho na mawakibu kimekamilisha maandalizi ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika taiafa la Iraq na ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimekamilisha maandalizi ya kupokea mazuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani na mawakibu za kutoa huduma, kimeweka mkakati maalum wa kurahisisha matembezi ya mazuwaru na kutoa huduma bora.

Rais wa kitengo Sayyid Aqiil Abdulhussein Alyaasiriy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maandalizi ya ziara hii yameanza mapema mwaka huu, yanahusisha vitu vingi ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo na kanuni kwa viongozi wa Mawakibu zitakazo shiriki kuhudumia mazuwaru wakati wa ziara, maukibu ambayo haijapata maelekezo na kanuni hizo hairuhusiwi kutoa huduma, jambo hilo ni muhimu na hufanywa na kituo kwa kushirikiana na idara ya usalama ya mkoa wa Karbala”.

Akabainisha kuwa: “Maandalizi huwa ya aina mbili, kwanza uratibu ambao hufanywa na idara yetu, pili ulinzi na usalama hufanywa na idara ya usalama, hivyo ni muhimu kwa viongozi wa mawakibu kupewa taratibu maalum kabla ya kuanza kutoa huduma, hasa Maukibu zinazotaka kutoa huduma ndani ya eneo la mkoa wa Karbala, au katika vitongoji na barabara zinazo elekea Karbala”.

Akafafanua kuwa: “Tumeainisha sehemu ya kila maukibu inapo takiwa kutolea huduma zake, sambamba na kuahidi kutekeleza maelekezo waliyo pewa, tutakua na kikosi cha ugagizi kitakacho tembelea kila Maukibu na kukagua utekelezaji wa kanuni tulizo kubaliana”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maadhimisho kinawajibika kuweka kanuni na kuratibu utendaji wa vikundi na Mawakibu Husseiniyya, sambamba na kutoa vitambulisho kwa viongozi wa Mawakibu, yoto hufanywa kwa kushirikiana na idara ya usalama
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: