Kazi kubwa ya usafi kwenye ukuta wa nje wa ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Wadumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanasafisha ukuta wa nje wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya utaratibu maalum uliowekwa.

Ufasi huu unafanywa karibu na mwezi kumi na tano Shabani, kufuatia ukuta huo kuchafuliwa na kimbunga cha udongo pamoja na uvunjaji wa majengo yaliyokua karibu na ukuta huo.

Kundi la wahudumu wa kitengo cha utumishi idara ya usafi limeshiriki kwenye kazi hiyo, wameanzia upande wa mlango wa Kibla hadi mwisho, usafi unafanywa kwa kutumia mitambo maalum, wameanza kusafisha sehemu ya juu yenye nakshi na mapambo hadi kwenye maandishi ya Qur’ani na sehemu ya chini, pamoja na kusafisha alama zilizopo juu ya kila mlango.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: