Chuo kikuu Al-Ameed kinafanya kongamano la mazazi la kila mwaka

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya kongamano la mazazi la kila mwaka, katika kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu wa zama (a.f), na kuhudhuriwa na kundi la wanafunzi na wakufunzi na baadhi wa viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kongamano limefunguliwa kwa Qur’ani, iliyosomwa na msomaji wa Ataba mbili tukufu Sayyid Hasanaini Halo, ukafuata ujumbe wa chuo ulio wasilishwa na makamo rais wa mambo ya utawala Dokta Alaa Mussawi, akaongea kuhusu utukufu wa Ahlulbait (a.s) na umuhimu wa kuhuisha kumbukumbu zao, na matukio haya kuwa chachu ya kurekebisha mazingira wanayo ishi wanaadamu kwa sasa.

Halafu ukafuata ujumbe elekezi kutoka kwa Mheshimiwa Shekhe Habibu Alkadhimi, akabainisha vipengele kadhaa vya kimalezi na kimaadili, akaeleza umuhimu wa kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s).

Kongamano limepambwa na mashairi kutoka kwa Muhammad Fatwimiy, yaliyo eleza kuhusu Imamu wa zama (a.f), pamoja mashairi kutoka kwa bwana Ammaar Alkinani.

Kongamano likahitimishwa kwa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa chuo waliovaa Abaa za kiiraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: