Rais wa wakfu Shia amesema: Kuna haja kubwa ya kupanua uwanja wa nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Rais wa wakfu Shia Dokta Haidari Shimri amesema, kuna haja kubwa ya kusaidia juhudi za Atabatu Abbasiyya za kupanua uwanja wa nje ya malalo takatifu, kwa kununua ardhi inayozunguka eneo hilo.

Akasema: “Upanuzi huo unahitaji msaada wa serikali, inatakiwa itenge kiwango cha pesa kutoka wizara ya fedha, kwa kushirikiana na wizara ya mipango sambamba na kusukumwa jambo hilo na bunge ili kupata msaada huo muhimu”.

Akaongeza kuwa: “Jambo la kununua ardhi hizo ni muhimu kwa miradi ya Atabatu Abbasiyya, aidha itasaidia kuwa na uwanja mkubwa wenye uwezo wa kuingiza mamilioni ya watu kila mwaka”.

Akasisitiza kuwa: “Wakfu Shia tutafanya kila tuwezalo kuiomba wizara ya fedha na kuwaomba wabunge wapitishe jambo hilo, ili Atabatu Abbasiyya iweze kununua nyumba hizo, na kutekeleza malengo yake”.

Kumbuka kuwa rais wa wakfu Shia, alitembelea maeneo ya Ataba tukufu akiwa pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na baadhi ya marais wa vitengo, akaangalia maeneo yanayo zunguka Ataba tukufu na ramani iliyo andaliwa na Ataba tukufu ya upanuzi wa malalo hiyo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: