Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya kongamano la kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Qaaimu Aali Muhammad Imamu Mahadi (a.f), ndani ya ukumbi wa kitivo cha uhandisi na teknolojia na kuhudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani, na baadhi ya wakuu wa vitivo na walimu na wanafunzi.
Kongamano hilo limeratibiwa na kitengo cha maelekezo ya nafsi na malezi, kwa kushirikiana na kitivo cha uhandisi na teknolojia na taasisi ya kiraia ya Najafu, hufanywa kila mwaka katika siku kama hizi.
Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha ukafuata ujumbe wa Ustadh Ali Jaasim Ramadhani mkuu wa kitivo cha uhandisi, ameeleza kuhusu umuhimu wa kuadhimisha matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), likiwemo tukio hili la kuzaliwa muokozi wa umma atayejaza dunia uadilifu na amani baada ya kujaa dhulma na uovu, akausia wahudhuriaji wafanye kongamano hili kuwa chachu ya maendeleo ya kielimu na ustawi wa jamii.
Baada ya hapo yakafuata mashairi na tenzi kuhusu tukio hilo tukufu, kutoka kwa wanafunzi wa chuo.
Mwisho wanafunzi wanaozingatia vazi la Abaa la kiiraq wanapokua chuoni wakapewa zawadi.