Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) inajiandaa kupokea mazuwaru

Maoni katika picha
Kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha maandalizi ya kupokea mazuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani.

Rais wa kitengo hicho Ustadh Adnani Dhaifu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara ya mwezi kumi na tano Shabani inaumuhimu mkubwa sana katika Maqaam hii, kutokana na uhusiano wake na mwenye tukio, hivyo huanza maandalizi mapema, huimarisha ulinzi na kuweka mazingira mazuri ya utoaji wa huduma kwa watu wanaokuja kutembelea sehemu hii tukufu katika mji wa Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Maandalizi yamehusisha ukarabati wa maeneo yote ya Maqaam tukufu, kuanzia kumbi za ndani na maeneo yote yanayo zunguka haram kwa nje, tumekarabati taa, viyoyozi, vipaza sauti na vinginevyo, pamoja na kuweka mapambo, mabango na mauwa”.

Akaendelea kusema: “Kuna utaratibu utakaofuatwa wakati wa ziara kwa ajili ya kurahisisha shughuli za mazuwaru na kupunguza msongamano, tutaweka vizuwizi na watu watakao simamia matembezi na kuhakikisha hautokei msongamano”.

Akasema: “Kuhusu maandalizi ya ulinzi na amani, tulifanya vikao na viongozi wa polisi, viongozi wa Ataba mbili tukufu na kikosi cha ulinzi wa haram mbili, na kuweka mikakati ya kuhakikisha ziara inakua ya amani na utulivu”.

Akamaliza kwa kusema: “Tumekamilisha maandalizi kwa kufanya hafla kubwa ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Qaaimu (a.s) katika mkoa wa Karbala, ya kongamano la mishumaa, ambalo hufanywa kila mwaka na kuhudhuriwa na watu wengi, sambamba na ushiriki wetu katika hafla itakayofanywa na Atabatu Husseiniyya tukufu katika uratibu na usimamizi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: