Mazingira ya furaha za kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.f) yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mazingira ya furaha yametanga kwenye maeneo yote ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kumbukumbu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa muokozi wa umma Imamu wa zama (a.s).

Tangu ulipo ingia mwezi mtukufu wa Shabani mazingira ya furaha yametanda katika haram tukufu, yamezidi kuongezeka katika tukio la kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu wa zama (a.f), idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya imeshona na kudarizi vitambaa vyenye jumbe nzuri za kuadhimisha mazazi haya matukufu.

Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu wameweka vitambaa hivyo kila sehemu ya ukumbi wa haram tukufu, sambamba na kuweka mauwa na mapambo kwenye milango yote ya Ataba takatifu.

Aidha wameweka shada za mauwa mazuri kwenye dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuyapanga katika muonekano mzuri wa kuvutia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: