Kukaribia kilele cha ziara ya mwezi kumi na tano Shabani na Atabatu Abbasiyya imeongeza utoaji wa huduma zake

Maoni katika picha
Mji mtukufu wa Karbala tangu asubuhi na mapema mamia kwa maelfu ya mazuwaru wamekuwa wakiwasiri kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Mahadi (a.f).

Idadi ya watu wanao wasili kutoka mikoa tofauti ya Iraq na baadhi ya nchi za kiarabu na kiajemi imekua ikiongezeka kidogo kidogo, na kilele chake ni siku ya mwezi kumi na tano Shabani.

Haram na ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) umefurika mazuwaru sambamba na kuimarishwa ulinzi na usalama pamoja na kuboreshwa kwa huduma zinazo tolewa na watumishi wa malalo takatifu, ambao wanafanya kila wawezalo kuhakikisha ziara inafanywa kwa amani na utulivu.

Kwa upande mwingine mawakibu za kutoa huduma zimeweka kambi kwenye barabara zote kubwa na ndogo, zinagawa chakula na kutoa huduma ya malazi kwa mazuwaru, katika mazingira salama yaliyojaa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: