Idara ya usimamizi wa haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea na shughuli za maandalizi ya ziara ya Shaabaniyya tukufu.
Watumishi wa idara wanafanya kazi kubwa ya kuratibu matembezi ya mazuwaru, ya kuingia na kutoka ndani ya haram tukufu, na kuwasaidia kufanya ziara kwa utulivu na amani.
Idara imeandaa kikosi cha watumishi waliopewa mafunzo ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza kwa kushirikiana na idara ya madaktari, kwa ajili ya kutoa msaada wa kiafya haraka pale utakapo hitajika, sambamba na kuendelea na kazi ya usafi wakati wote.
Kazi hii inafanywa kwa kushirikiana na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu saa 24 kila siku.
Tambua kuwa idara inayosimamia haram tukufu huandaa utaratibu maalum wakati wa ziara ya Shaabaniyya kila mwaka, na kilele cha ratiba yao ni wakati kama huu.
Kumbuka kuwa idara inayosimamia haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanya kazi kubwa wakati wa ziara ninazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ikiwemo ziara hii ya Shaabaniyya.