Watumishi wa kulinda nidhamu wameimarisha ulinzi na nidhamu katika ziara ya Shaabaniyya

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha kulinda nidhamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu wametekeleza wajibu wao kwa weledi mkubwa katika ziara ya Shaabaniyya, wameimarisha ulinzi kwa mazuwaru na kusimamia harakati zao.

Wamefanya kazi ya upekuzi wa watu na mabeji kwenye vituo maalum vya ukaguzi vilivyo wekwa katika barabara zinazoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa umakini mkubwa.

Aidha kitengo cha upelelezi kimefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi, kwa lengo la kulinda usalama wa mazuwaru na mali zao.

Wanafanya kazi muda wote kwa kushirikiana na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya pamoja na wahudumu wa kujitolea waliokuja kutoka mikoa tofauti.

Kumbuka kuwa kitengo cha kulinda nidhamu ni sawa na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanya kila wawezalo kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake mnyweshaji wenye kiu Karbala (a.s) katika ziara hii na ziara zingine kubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: