Kazi kubwa imefanywa na kitengo cha usimamizi wa haram katika ziara ya Shabaniyya

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya wamefanya kazi kubwa ya kuwahudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kipindi cha ziara ya Shaabaniyya.

Miongoni mwa kazi zao ni kuongoza matembezi ya mazuwaru wakati wa kuingia na kutoka ndani ya haram tukufu, kuandaa sehemu za kuswalia na kutenga sehemu ya chini ya haram kwa ajili ya wanawake.

Walianza na kazi ya kusafisha sehemu zote za haram tukufu, pamoja na kupuliza marashi na kuweka idadi kubwa ya vitabu vya ziara na turba kwenye shelfu za vitu hivyo.

Tambua kuwa kitengo cha kusimamia haram kinakazi maalum katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile kupiga deki, kusafisha mazulia na zinginezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: