Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa gari kwa ajili ya kubeba mazuwaru wa Shaabaniyya

Maoni katika picha
Kitengo cha mitambo katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa zaidi ya gari (150) zenye ukubwa tofauti kwa ajili ya kushiriki kwenye zowezi la kubeba mazuwaru.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Abduljawaad Kaadhim Abbasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maandalizi ya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani yalianza mapema, kitengo chetu kimeandaa gari za ukubwa tofauti, kwa ajili ya kurahisisha uingiaji na utokaji wa mazuwaru katika mji wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Tumeandaa gari za wagonjwa pia kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu, na gari za maji, ambazo zinajukumu la kugawa maji kwa mawakibu zinazotoa huduma na maeneo yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya na kwenye vituo vya polisi”.

Akabainisha kuwa: “Gari zinazo shiriki kubeba mazuwaru zipo (120 zenye uwezo wa kubeba abiria 28) na basi (20 zenye uwezo wa kubeba watu 48), kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa, tunatoa huduma katika barabara ya (Baabil – Karbala), ambayo hutumiwa na idadi kubwa ya mazuwaru”.

Akamaliza kwa kusema: “Programu hii imehusisha kikosi cha mafundi makenika wenye jukumu la kutengeneza gari yeyote itakayoharibika wakati wa kazi papo hapo, bila kwenda kwenye gereji za kitengo, hali kadhalika madereva wamepangwa katika zamu mbili, zamu ya jioni na asubuhi, sambamba na kuandaa kituo cha kuanzia safari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: