Kitengo cha katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, kimesema kuwa: baada ya kumaliza maandalizi ya ziara ya Shaabaniyya, wameanza utekelezaji wa kutoa huduma rasmi.
Rais wa kitengo tajwa Sayyid Naafii ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu walianza kutoa huduma chini ya utaratibu maalum uliopangwa katika ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani, wamefanya kila wawezalo katika kuweka mazingira ya amani na utulivu katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu pamoja na kusimamia matembezi ya mazuwaru”.
Akaongeza kuwa: “Idara za kutoa huduma zinafanya kazi wakati wote, utawakuta wanafagia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu muda wote na barabara zinazo zunguka eneo hilo, wanagawa maji kwa mawakibu na mazuwaru, na kuongoza matembezi ya mawakibu na mazuwaru wakati wote”.
Akabainisha kuwa: “Watumishi wetu wa idara ya Habari watarahisisha matangazo ya shughuli za ziara zinazo fanyika katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na kuyatoa kwa vyombo vyote vya Habari vinavyo penda kurusha matukio ya ziara”.
Akasisitiza kuwa: “Kazi haitaishia siku ya kumi na tano ya mwezi wa Shabani, bali siku hiyo itashuhudia kazi nyingi, na baada ya kumaliza ziara maalum ya siku hiyo, tutaanza kazi ya kusafisha mji wote wa Karbala”.