Wahudumu wa mazuwaru katika Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kufanya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani baada ya kumaliza kuhudumia mazuwaru wa Shaabaniyya.
Wahudumu wa sekta mbalimbali kama vile afya, ulinzi, uratibu na zinginezo, wamekusanyika ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufanya ziara, walipo maliza wakaenda kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) huku wakiimba kaswida na kusoma tenzi za kuadhimisha mazazi ya Imamu wa zama (a.f).
Walipo wasili katika Atabatu Husseiniyya wamefanya ibada ya ziara pamoja na mazuwaru wengine.
Kumbuka kuwa wahudumu wa kujitolea wamekuja kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kwa lengo la kuwahudumia mazuwaru wa Shaabaniyya bega kwa bega pamoja na watumishi wa Ataba mbili tukufu kwenye sekta mbalimbali.