Kituo cha turathi za Hilla chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya hafla ya kupongeza ushindi wa vitabu vyake vitatu kwenye shindano la kongamano la kitabu bora cha hauza katika mwaka, lililofanywa katika mji wa Qum sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu (a.f).
Hafla imefanywa ndani ya ukumbi wa Ameed katika mji wa Hilla, hafla ilikua na vipengele vingi, kama vile usomaji wa Qur’ani tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kurehemu mashahidi wa Iraq, ukafuata ujumbe wa makaribisho uliotolewa na Dokta Ahmadi Rashidi Didah, na mhadhara wa kidini ukatolewa na Sayyid Abu Dhari unaohusu kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu wa zama (a.f).
Aidha hafla ilipambwa na usomaji wa mashairi.
Mwisho ukawasilishwa muhtasari wa vitabu vilivyo shinda na Dokta Ali A’araji, akabainisha hatua muhimu zilizopitiwa na vitabu vilivyo shinda.
Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinajukumu la kufanya uhakiki na uandishi wa vitabu, kinaidara mbalimbali zinazofanya kazi kwa weledi mkubwa.