Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mradi wake wa (kuza kipaji) kwa kushirikiana na kikosi cha Abbasi (a.s), kipo katika hatua za kwanza za kuandaa tukio la kuwaenzi watu waliopata shahada (uawa) kwa ajili ya kulinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu, kwa wakufunzi wa vyuo na wanafunzi wao,
Kiongozi mtendaji wa mradi huo (kuza kipaji) Ustadh Omari Ulaa ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Fikra ya mradi huu imetokana na fikra ya kuadhimisha mwaka wa nane tangu ilipotolewa fatwa tukufu ya kujilinda, kwa kufanya tukio la kuwaenzi mashahidi katika vyuo vikuu vya Iraq baada ya kupewa kibali rasmi cha kuandaa kazi za kiufundi zitakazo ambatana na kuandika majina ya wakufunzi na wanafunzi walioitikia wito wa taifa na Marjaa, wakajitolea damu zao kwa ajili ya kulinda taifa hili na maeneo matakatifu, pamoja na kubandika picha zao, majina yao, wasifu wao na sehemu walipo pata shahada”.
Akaongeza kuwa: “Hii ni kazi ya kwanza kufanywa katika mfumo huo hapa Iraq, ni sehemu ya kuenzi damu zao takatifu na kujitolea kwao kutukufu, sambamba na kupongeza kazi kubwa waliyo fanya wao na familia zao, aidha ni kuwakumbusha walimu na wanafunzi kazi zilizofanywa na wenzao katika kulinda taifa la Iraq”.
Naye kiongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) amesema kuwa, fikra hii ni muhimu sana, inalenga kudumisha fatwa tukufu iliyotolewa na Mheshimiwa Marjaa mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani iliyo okoa Iraq na kudumisha kumbukumbu ya mashahidi waliojitolea kila wanacho miliki kwa ajili ya kulinda taifa, na kuwafanya waendelee kukumbukwa na vizazi vijavyo.