Safari ya kidini na kitamaduni kwa wanafunzi wa kuhifadhi Qur’ani katika mkoa wa Najafu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imeandaa safari ya kidini kwa wanafunzi walioshiriki kwenye semina ya kuhifadhi Qur’ani tukufu.

Mkuu wa Maahadi Ustadh Muhandi Almayali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Safari imesimamiwa na walimu wa Maahadi, ratiba ya safari imehusisha kutembelea malalo ya Imamu Ali (a.s) na kusoma ziara na dua kwa pamoja, sambamba na kutembelea maeneo mbalimbali ya haram hiyo takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Kisha tulienda katika kituo cha Muhsin chini ya Atabatu Alawiyya, wanafunzi wakapata nafasi ya kufanya mazowezi na kujisomea, wakiwa katika kituo hicho wamefanya mashindano ya usomaji wa Qur’ani baina yao, wamefanya maigizo na kushiriki kwenye michezo mbalimbali, na wakaangalia majarida na vitabu tofauti katika maktaba ya kituo, kisha wakaelekea katika mgahawa wa Imamu Ali (a.s) kwa ajili ya chakula cha mchana”.

Akaendelea kusema: “Ratiba hii imefanywa kwa ajili ya kuwapa mapumziko wanafunzi hao watukufu, na kuwajengea mapenzi ya Ahlulbait (a.s), sambamba na kuwajengea hulka ya kusaidiana baina yao, tunaamini kuwa safari za aina hii huongeza moyo wa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: