Chuo kikuu Alkafeel kimefanya hafla ya Mahdawiyya

Maoni katika picha
Kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya hafla ya kuhuisha kuzaliwa kwa Imamu wa zama (a.f).

Hafla imefanya chini ya usimamizi wa rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani kwa kushirikiana na taasisi ya Najafu ndani ya ukumbi wa chuo na kuhudhuriwa na wakufunzi wa udaktari na wanafunzi wa chuo.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata ujumbe kutoka kwa uongozi wa chuo ulio wasilishwa na Nawaal Aaidi Almayali, ametoa pongezi za kuadhimisha tukio hili tukufu, akakumbusha misingi tunayotakiwa kuifuata kwa ajili ya kupata radhi za Imamu wa zama (a.f) katika zama za Ghaiba, akahimiza wahudhuriaji kushikamana na swala hili la kiimani sambamba na kulifanya kuwa msingi muhimu katika maisha yetu na jamii zetu.

Hafla imepambwa na mawaidha na kaswida kutoka kwa wanafunzi zilizo husu kumpenda Imamu wa zama (a.f), na kusomwa kwa pamoja dua ya Faraj, aidha kulikua na kipengele cha maswali na majibu yaliyojikita katika historia ya Imamu na ghaiba yake.

Hili ni moja ya matukio yanayo pewa umuhimu na chuo, kwani linafundisha kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s) na kunufaika katika sekta ya elimu na kazi.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kupitia kitengo cha maelekezo ya kinafsi na kimalezi huadhimisha matukio ya Ahlulbait (a.s), chini ya ratiba maalum ambayo huwa na vipengele vingi vinavyo husu tukio husika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: