Kituo kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya kimeandaa hafla ya Mahdawiyya kwa wanafunzi wa Dini wa kiafrika

Maoni katika picha
Kituo cha Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Imamu Hujjat msubiriwa (a.f), kwa kushirikiana na umoja wa wanafunzi wa mtumishi wa Ahlulbait (a.s) Shekhe Ibrahim Zakzaki, na kuhudhuriwa na kundi la wanafunzi wa Dini wa Afrika.

Hafla imefanywa ndani ya ukumbi wa kituo katika mkoa wa Najafu, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo fuatiwa na ujumbe kutoka kwa waandalizi wa hafla ulio wasilishwa na Sayyid Muslim Aljaabiriy, alianza kwa kutoa mkono wa pongenzi kwa wahudhuriaji kwa kuadhimisha tukio hili tukufu, akahimiza umuhimu wa hafla hiyo na kuifanya kuwa chachu ya kushikamana na Imamu Mahadi (a.f), na kujipanua zaidi katika kumtambua na kufuata mwenendo wake, hakika yeye ni moja ya sehemu muhimu ya kiitikadi.

Baada yake ukafuata ujumbe wa umoja wa wanafunzi uliowasilishwa na Shekhe Ahmadi Muaadh, akaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na kituo cha Dirasaati Afriqiyya kwa kufanya hafla hii pamoja na misaada wanayotoa kwa wanafunzi wa Dini wa kiafrika, halafu ukafuata ujumbe wa mgeni rasmi ulio wasilishwa na Sayyid Abdulmutwalib Mussawi, akaongea mambo mengi yanayo husu Imamu Mahadi (a.s).

Kisha Shekhe Muhammad Raabii Balo akasoma nasaha za Shekhe Zakzaki kwa wanafunzi wa kiafrika.

Hafla ikapambwa na mashairi na tenzi zilizo somwa na vikundi viwili vya kaswida vya wanafunzi wa kiafrika kutoka Karbala na Najafu.

Mwisho wa hafla kiongozi wa muungano wa wanafunzi wa kiafrika Shekhe Zainul-Aabidina Abdallah, akatoa shukrani kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kituo kwa kuandaa hafla za kuadhimisha matukio ya kidini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: