Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa zawadi kwa majeruhi wa fatwa ya kujilinda, leo siku ya Ijumaa mwezi (20 Shabani 1443h) sawa na tarehe (25 Machi 2022m) baada ya Adhuhuri.
Zawadi zimetolewa katika hafla iliyofanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (kuwatendea haki mashahidi walio hai) ndani ya ukumbi wa jengo la Shekhe Kuleini chini ya Atabatu Abbasiyya na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo, bila kusahau viongozi mbalimbali na watu walio jeruhiwa wakati wakitekeleza maelekezo ya fatwa tukufu ya kujilinda pamoja na familia zao.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo somwa na Sayyid Haidari Jalikhani, kisha ikasomwa rurat Fatha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ukafuata wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa).
Halafu ukafuata ujumbe kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.
Baada yake kukawa na ujumbe kutoka kwa majeruhi waliopewa zawadi uliowasilishwa na Sayyid Rasuul Mussawi, akasema: “Ndugu zangu vita ya leo ni kali sana, nayo ni vija isiyo ya wazi, na sababu zake ziko wazi, na adui yuko wazi, hatuna vifaa vya kutuwezesha kushinda ispokua kushikamana na wanachuoni wa kweli na sio vinginevyo, kuna baadhi wanajifanya wanaelimu wakati hawana elimu yeyote, hakika tupo katika wakati mgumu na muhimu, tumepewa jina la Hashu-Sha’abi kwa sababu ya kuitikia wito wa jihadi kifaya ya kujilinda, tunatakiwa kuendelea kufanyia kazi maelekezo ya wanachuoni, hasa maelekezo ya Mheshimiwa Sayyid Sistani”.
Akaongeza kuwa: “Hakika Marjaa huyu tunatakiwa tusimame nyuma yake kwa dhati, tusidanganywe na Dunia, Dini ndio yenye thamani, mwanaadamu anatakiwa ajitolee kila kitu ispokua Dini”.
Akaendelea kusema: “Kwa ajili gani zilimwagika damu tukufu vitani? Ni kwa ajili ya Dini na vita vyote vilivyo piganwa katika madhehemu kuanzia alipo uawa kiongozi wa waumini hadi leo ni kwa ajili ya Dini, Dini yetu imenyeshelezwa kwa damu ya Maimamu watakasifu na wanachuoni watukufu, tumekuja hapa kuadhimisha jinsi watu walivyo itikia wito wa Marjaa Dini mkuu”.
Hafla imepambwa na mashairi kutoka kwa Ali Swafaar Karbalai na kutoka kwa Ali Swahibu A’ajibiy na Muhammad Hashimi, wakamalizia kwa kuonyesha filamu fupi inayo onyesha moja ya tukio la kukomboa ardhi ya Iraq iliyokua imetekwa na magaidi wa Daesh, hafla ikahitimishwa kwa kugawa zawadi kwa majeruhi.