Chuo kikuu Alkafeel kinafanya kongamano la kielimu la kwanza kwa wanafunzi wa udaktari wa meno

Maoni katika picha
Kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya kongamano la kielimu la kwanza kuhusu tiba ya maeno, kwa ajili ya kusaidia wahitimu wapya katika tiba hiyo, na kuangalia uwezo wao katika swala hilo.

Kongamano limefanywa siku ya Ijumaa (21 Shabani 1443h) sawa na tarehe (25 Machi 2022m) kwenye jengo la kitivo cha ufamasia katika chuo kikuu cha Alkafeel, chini ya usimamizi wa rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani na kuhudhuriwa na wakuu wa vitivo vya udaktari wa meno na vyuo vingine pamoja na wasaidizi wao na baadhi ya viongozi wa sekta ya tiba na wanafunzi.

Kongamano limehusisha maonyesho ya maswala ya tiba, kupitia mihadhara na warsha iliyohutubiwa na wahitimu wa kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel, miongoni mwa wahadhiri ni:

  • - Daktari bingwa wa meno Zaidu Ali Mussawi, mada yake inaitwa: Challenges in Sinus Lif.
  • - Daktari wa meno Muhammad Mussawi, mada yake inaitwa: Digital Smile Desing in Daily Clinical Practice.
  • - Daktari wa meno Hussein Ali Alhusseiniy, mada yake inaitwa: Restoration of Endodontically Treated Teeth: More Conservative & Better Outcome.
  • - Daktari bingwa wa meno Amiir Yusufu Anuuz, mada yake inaitwa: Indirect Restoration from Prosthodontist Point of View.
  • - Daktari wa meno Zainul-Aabidina Sajjaad, mada yake inaitwa: Optimizing Proximal Posterior Composite Restoration.

Mkuu wa kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Karim Maktufu akasema: “Kongamano la wahitimu wa kitivo cha udaktari wa meno, linaumuhimu mkubwa katika chuo, kwani linamsaada mkubwa kwa wanafunzi na wahitimu, husaidia kubadilishana uzowefu wao, katika kufanyia kazi yale waliyosoma kwa nadhariyya wakiwa darasani, hivyo kongamono hili ni uwanja wa kupanuana mawazo na kubadilishana uzowefu, sambamba na kuangalia mbinu za kisasa zinazo tumika katika kutibu meno”.

Wanafunzi waliohitimu wamepongeza kazi nzuri iliyofanywa na uongozi wa chuo Pamoja na wakufunzi, ya kuwakutanisha na kuwaendeleza kielimu, sambamba na maendeleo ya kisasa yanayo patikana katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: