Mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu: washindi wa shindano la (Dhawaati himam) la kuhifadhi Qur’ani kwa wasichana wamepewa zawadi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu mbele ya kiongozi wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu, imetoa zawadi kwa washindi watano wa shindano la (Dhawaati himam) la kuhifadhi Qur’ani maudhui kwa wasichana, lililoandaliwa na kitengo cha masomo ya Qur’ani chini ya chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sayyid Swafi amepongeza washindi na wazazi wao kwa mafanikio hayo ambayo yanawafanya kuwa kigezo chema katika jamii, akasema: “Tunajivunia juhudi zenu na kufaulu kwenu, watu wengine wanatakiwa kujifunza kwenu”, akaongeza kuwa: “Nyie mnafurahi kwa kupewa zawadi na sisi tunafuraha kwa ushiriki wenu kwenye shindano hili kwa hakika hakuna aliyeshindwa na mshindi, madam mmefungamana na Qur’ani tukufu na kizazi kitakatifu”.

Akasema: “Mwanaadamu anaposoma Qur’ani huwa sawa na anaongeleshwa na Mwenyezi Mungu, bila shaka hakuna maneno mazuri zaidi kushinda maneno ya Mwenyezi Mungu, na nyie pia muongee na Mwenyezi Mungu, kama yeye anavyo ongea na mja hutaka pia mja aongee nae”.

Rais wa kitengo cha masomo ya Qur’ani Ustadh Ali Bayati ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano limeandaliwa na kufadhiliwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nalo ni miongoni mwa mashindano ambayo hufanywa na kitengo cha masomo ya Qur’ani katika chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) katika mji wa Najafu, ni shindano adimu katika taifa la Iraq, kuhifadhi Qur’ani maudhui kunaumuhimu mkubwa kwa mtu na jamii, hususan kwa wale wasioweza kuhifadhi Qur’ani yote”.

Akaongeza kuwa: “Shindano limeandaliwa kulingana na kiwango cha washindani, chini ya usimamizi wa kamati ya majaji, washiriki wametoka mikoa tofauti ya Iraq, na limefanywa kupitia mtandao wa (Google Meet), sambamba na ushiriki wa taasisi ya Alkafeef Alqur’aniyya, mbele ya kamati ya majaji waliobobea katika sekta ya hifdhu maudhui.

Wafuatoa ni washindi watano wa shindano hilo:

Mshindi wa kwanza: Ruqiyya Adiiib/ kutoka Bagdad.

Mshindi wa pili: Aayah Imaad/ kutoka Diyala.

Mshindi wa tatu: Dhiyaau/ kutoka Bagdad.

Mshindi wa nne: Fatuma Muhammad/ kutoka Basra.

Mshindi wa tano: Hanani Muftini/ kutoka Basra”.

Naye rais wa taasisi ya Alkafeef ya Qur’ani Dokta Wasaam Khuz’aliy, akatoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufanya jambo hili la pekee, na akaomba ratiba iendelee kwa vijana wa umri tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: