Kundi la wanafunzi kutoka vyuo vikuu vitatu sehemu ya sherehe za kuhitimu kwao wanafanyia katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kundi la wanafunzi kutoka vyuo vikuu vitatu (Kufa, Ibun Hayaan na Alkafeel), sehemu ya sherehe za kuhitimu kwao wamefanyia ndani ya haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya ratiba iliyo andaliwa na idara ya mahusiano ya vyuo chini ya kitengo cha mahusiano katika Ataba tukufu.

Ratiba ilikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kutembelea sehemu za Ataba hiyo tukufu pamoja na kutembelea makumbusho ya Alkafeel, maktaba na Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya, wametambua mambo mengi na utendaji wake.

Ugeni huo baada ya kumaliza kutembelea maeneo ya Atabatu Abbasiyya ukaelekea katika Atabatu Husseiniyya, wakafanya ziara mbele ya malalo ya Abu Abdillahi Husseini (a.s), wakiwa pamoja na watumishi wa malalo hiyo takatifu.

Kisha wakafanya kikao ndani ya ukumbi wa Imamu Hussein (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wakasikiliza mada elekezi iliyotolewa na mjumbe wa kitengo cha Dini Sayyid Muhammad Abdullahi Mussawi.

Mwisho wahitimu wakala kiapo kwa taifa na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na uaminifu, kisha wakapewa zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Wanafunzi wameshukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu na wasimamizi wa ratiba hii, wakasema kuwa tukio hili litakua taa linaloangazia maisha yao na safari yao ya kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: