Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa, kimegawa sahani za chakula (3,062,828) milioni tatu elfu sitini na mbili mia nane ishirini na nane, katika mwaka wa 2021m, kwa mazuwaru waliokuja kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Rais wa kitengo tajwa Mhandisi Aadil Hamaami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ugawaji wa chakula unaofanywa na mgahawa ulianza miaka iliyopita, na kila mwaka umekua ukiongezeka sambamba na kuongezeka vifaa na wahudumu pamoja na ubora wa huduma zinazotolewa”.
Akaongeza kuwa: “Asilimia kubwa ya chakula kimegawiwa kwa mazuwaru wa Arubaini, zaidi ya sahani milioni moja na miambili ziligawiwa wakati wa ziara iliyopita, pamoja na misimu mingine ya ziara, kama mwezi kumi muharam, siku ya Arafa na mwezi mtukufu wa Ramadhani na siku za Ijumaa na matukio mengine ambayo huadhimishwa hapa Karbala kama vile tarehe za kuzaliwa na kufariki kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), bila kusahau chakula ambacho hugawiwa kwa vikosi vya ulinzi na usalama na wahudumu wa kujitolea katika Ataba tukufu na makundi mengine”.
Akafafanua kuwa: “Uandaaji wa chakula huzingatia mahitaji ya mazuwaru, sambamba na ugawaji wa juisi, matunda, halwa na vitafunwa vingine”. Akasema kuwa: “Chakula hugawiwa kupitia maeneo manne ambayo huwa na mazuwaru wengi, bila kusahau kwenye kumbi kuu za mgahawa, sehemu zote chakula hugawiwa kwa utaratibu mzuri bila kusababisha msongamano wa watu”.
Akamaliza kwa kusema: “Mwaka huu tumejiandaa mapema na mpango kazi utakuwa wa wazi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na baraka za tunaemtumikia, na msaada usiokua na kikomo tunaopata kutoka kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo wakati wote inahakikisha mazuwaru wanapewa huduma bora zaidi”