Mkuu wa kituo Ustadh Ali Jayashi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huduma hii ni sehemu ya mkakati wa uboreshaji wa App, nao ni utambuzi wa muda ambao unaweza kunufaika nao kwa kutambua nyakati za swala, wakati wa kufuturu na kuanza kwa funga, kulingana na jografia ya kila eneo”.
Akaongeza kuwa: “Huduma hii imeanza kutolewa muda mrefu, kupitia jopo la wataalamu wanaofanya kati katika App, kwa kila anayetaka kuitumia aingie kwenye ukurasa maalum na aandike jina la mji, ataona wakati wa kuanza funga na nyakati zingine kwa urahisi, App hii itamtosheleza na hatahitaji kutafuta taarifa kwenye mitandao isiyoaminika”.
Akasisitiza kuwa: “Inazingatiwa kuwa huduma ya kwanza ya aina hii katika ulimwengu wa kiislamu, inasifa zifuatazo:
- - Rahisi kuitumia.
- - Unaweza kuchagua rangi unayotaka.
- - Unaweza kuipakua kwa urahisi.
- - Unaweza kuchapisha kwa kiwango kizuri na ukubwa wowote unaotaka.
- - Uhakika wa wakati kulingana na kila eneo au mji.
- - Unaweza kutuma kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii”.
Kumbuka kuwa tangu kuanzishwa kwa App mwaka (2014m), kikosi kinacho simamia kimekua kikiifanyia maboresho kila wakati, kulingana na maendeleo yanayopatikana katika sekta hiyo, hadi imekua App bora katika App za kiislamu, takwimu zinaonyesha imezishinda App nyingi za mfano wake, hii inatokana na mikakati yake ambayo imeweza kufikia mahitaji mengi ya waislamu duniani.