Idara ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kwenye hafla ya kutimiza umri wa kuwajibikiwa kisheria kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya Laadhiqiyya ya wasichana katika mkoa wa Karbala.
Idara ya Qur’ani imekua na ushiriki kwa kufanya shindano la kifiqhi kwa wanafunzi hao, lenye lengo la kuwajulisha baadhi ya hukumu za kifiqhi zinazo endana na umri wao, sambamba na kutoa zawadi.
Uongozi wa shule ya Laadhiqiyya umeishukuru sana idara ya Qur’ani, kwa kuitikia wito na kuhudhuria kwake, jambo ambalo limewafurahisha wanafunzi wote na wazazi wao, wakaomba ushirikiano uendelee kati ya idara ya Qur’ani na shule.
Kumbuka kuwa harakati za idara ya Qur’ani zinalenga kuwajenga wasichana kitamaduni na kielimu.