Kuhitimisha vikao vya kongamano la kuthibitisha jinai na vitendo vya kigaidi vilivyo fanywa Iraq

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya Jumanne kimefanywa kikao cha nne na cha mwisho, katika kongamano maalum la kwanza liitwalo (Kuthibitisha jinai na vitendo vya ugaidi vilivyofanywa Iraq, mfumo wake, zana zake na changamoto zake).

Kikao cha mwisho kimefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kusimamiwa na Dokta Muhammad Kaadhim Kamar kutoka chuo cha Imamu Alkadhim (a.s), mada zilizo wasilishwa ni:

  • - (Kuthibitisha na faharasi ya jinai na misimamo mikali, changamoto za vipimo na mikakati ya ugaidi na mazingira), iliwasilishwa na Ustadh Ubaidu Alhaadi Ma’tuuq Alhaatimi.
  • - (Kumbukumbu ya wananchi na nafasi yake katika kuthibitisha jinai na ugaidi), imewasilishwa na Dokta Raaid Abisi kutoka kituo cha kuthibitisha jinai cha Iraq.
  • - (Kuthibitisha jinai za Watoto na mauaji ya halaiki kwa ajili ya kuzuwia yasijirudie), imewasilishwa na Dokta Hunzi Amiin Hassan Musaaid, rais wa chuo kikuu cha Jarmu cha mambo ya kiutawala.

Tambua kuwa kongamano limesimamiwa na kituo cha kuthibitisha jinai na ugaidi uliofanywa Iraq, chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na kituo cha Mulla cha utafiti katika chuo kikuu cha Koya.

Kumbuka kuwa kongamano linalenga kubadilishana uzowefu na kuunganisha nguvu, katika kuthibitisha jinai na mateso waliyopata raia wa Iraq, na kuangalia selebasi za kielimu katika kuthibitisha jinai na ugaidi, na kufuata mfumo sahihi pamoja na kuangalia changamoto zinazo patikana katika kazi ya uthibitishaji na kupendekeza njia za kuzitatua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: