Kongamano la kuthibitisha jinai na ugaidi uliofanywa Iraq limetoa maazimio kadhaa

Maoni katika picha
Alasiri ya Jumanne limehitimishwa kongamano la kitafiti la kwanza lililopewa jina la (Kuthibitisha jinai na ugaidi uliofanywa Iraq: mfumo wake, zana zake na changamoto zake), lililosimamiwa na kituo cha kuthibitisha jinai na ugaidi cha Iraq chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na kituo cha Mulla cha tafiti katika chuo kikuu cha Koya.

Kikao cha mwisho kimeorodhesha maazimio yaliyo tolewa na washiriki wa kongamano hilo, yamesomwa na rais wa kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Aqiil Abdulhusein Alyaasiriy, kama ifuatavyo:

  • 1- Umuhimu wa kushirikiana baina ya serikali na vituo vya tafiti vinavyo husika na kuthibitisha jinai na vitendo vya ugaudi, ili kurahisisha utendaji wao.
  • 2- Kuvipa nafasi vyuo vikuu vya Iraq ya kuthibitisha jinai na vitendo vya ugaidi vilivyo vyanywa Iraq, kwa kuandika vitabu na tafiti za kielimu sambamba na kufanya nadwa, warsha na makongamano.
  • 3- Kuunda kamati itakayo jumuisha wajumbe kutoka wizarati na kwenye taasisi za kiraia pamoja na vituo vinavyo fanya kazi ya kuthibitisha jinai na vitendo vya ugaidi.
  • 4- Kufanya kongamano maalum la kitaifa kwa ajili ya kuthibitisha jinai na vitendo vya kigaidi.
  • 5- Kufanya mashindano ya kitabu bora cha kuthibitisha jinai na vitendo vya kigaidi, na mashindano ya filamu bora, na picha bora na bango bora.
  • 6- Kongamano hili lifanywe kila mwaka sambamba na matukio ya kielimu.

Mwisho washiriki wa kongamano wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: