Kaimu balozi wa Norwey nchini Iraq Mheshimiwa Eriki Baja Husam amesema, shule za Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu zinamfumo mzuri wa elimu katika ngazi zote, ameyasema hayo alipotembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia miradi ya kimkakati.
Mheshimiwa Eriki Baja Husam akasema: “Shule za Al-Ameed zinamajengo mazuri kwa wanafunzi, jambo hilo linaonyesha umakini wa wasimamizi”. Akaonyesha kufurahishwa na utaratibu wote wa chuo kwa ujumla.
Rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Ahmadi Swabihi Kaabi amesema kuwa: “Kaimu balozi wa Norwey ameonyesha kufurahishwa na mazingira ya shule upande wa majengo na mfumo wa elimu, katika ziara yake ameangalia mfumo wa utawala na elimu unaotumika katika shule hizi”.
Akasema kuwa ubalozi wa Norwey unatambua kuwa Iraq ni taifa lenye jamii inayopenda kusoma na maendeleo, aidha kuna ushirikiano mzuri kati ya serikali na taasisi za kiraia katika nyanja tofauti za kiuchumi, kielimu na kidini.