Mafanikio makubwa katika kubadilisha viungo kwenye hospitali ya Alkafeel

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limesema kuwa kazi ya kubadilisha viungo imekua ikifanyika vizuri, imekua na mafanikio makubwa katika kutibu wagonjwa na kumaliza matatizo yao.

Daktari bingwa wa mifupa na viungo Dokta Ihsaani Faraji, amesema kuwa: “Upasuaji wa kubadilisha viungo umekua ukifanywa mara nyingi katika hospitali ya rufaa Alkafeel, kutokana na kuwepo vifaa-tiba vya kisasa kwenye vyumba vya upasuaji, sambamba na uwepo wa madaktari wenye weledi mkubwa”, akasema kuwa: “Matibabu ya ute wa goti yanayotolewa yanamuwezesha mgonjwa kutembea baada ya saa (24) tuko kuwekewa”.

Akasisitiza kuwa: “Vifaa tiba vilivyopo hasa vinavyo tumika katika upasuaji vinakubalika kimataifa”. Akasema kuwa: “Mafanikio yanayopatikana ni mengi, tumefanikiwa kuponya wagonjwa wengi”.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa na mahiri kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel kualika madaktari bingwa wa maradhi tofauti kutoka kila sehemu ya dunia, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: