Taasisi ya Yatima imesema: Atabatu Abbasiyya tukufu ipo mstari wa mbele katika kuendeleza vijana na kuwalea

Maoni katika picha
Ugeni kutoka mradi wa (Komaza kipaji), moja ya miradi inayofanywa na kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, umetembelea ofisi za taasisi ya mayatima katika mkoa wa Najafu na kukutana na kiongozi mkuu Sayyid Muhammad Hussein Alhakiim, kwa ajili ya kujadili namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano baina ya pande mbili.

Mkuu wa mradi Ustadh Omari Ula Alkifaaiy aneuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara yetu katika taasisi hii ni sehemu ya ziara nyingi tulizo fanya kwa taasisi zinazolea mayatima, kwa lengo la kuwaonyesha malengo ya mradi na jinsi ya kutekeleza vipengele vyake, kwa namna ambayo itasaidia kutoa huduma bora kwa mayatima na kuibua vipaji vya pamoja na kuviendeleza”.

Akaongeza kuwa: “Tumekubaliana kuchukua sampuni za baadhi ya vipaji vinavyo lelewa na taasisi, na kuviendeleza kama ilivyo pangwa na mradi”.

Akabainisha kuwa: “Sayyid Hakiim amepongeza mradi huu na kuusifu, akasema kuwa yuko tayali kusaidia ili kufanikisha malengo ya mradi, kwani kuendeleza vipaji vya mayatima ni jambo muhimu, akasema kuwa Atabatu Abbasiyya iko mstari wa mbele katika kuendeleza vijana na kulea vipaji vyao, aidha akatoa shukrani za dhati kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi kwa msaada wake katika swala hili”.

Akamaliza kwa kusema: “Mheshimiwa Sayyid Hakiim ameongea mambo mengi na akasisitiza utatuzi wa matatizo ya kijamii waliyonayo baadhi ya mayatima, na kuangalia harakati za vyombo vya Harari jinsi vinavyo ripoti vipaji vilivyo ubuliwa, na kuweka mikakati ya sasa na baadae katika kuboresha vipaji vya mayatima”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: